Pular para o conteúdo
Publicidade

2 Reis 4

Elisha amsaidia mjane

1 1 Fal 20:35;2 Fal 2:3-7;Kut 21:2;Law 25:39;Kum 15:12-18;Neh 5:1-13;Yer 34:8-18;Mt 18:25Basi, mwanamke mmoja miongoni mwa wake za wana wa manabii alimlilia Elisha, akasema, Mtumishi wako mume wangu amekufa; nawe unajua ya kuwa mtumishi wako alikuwa mcha BWANA; na aliyemdai amekuja ili ajitwalie wana wangu wawili kuwa watumwa. 2 1 Fal 17:12Elisha akamwambia, Nikufanyie nini? Niambie; una kitu gani nyumbani? Akasema, Mimi mjakazi wako sina kitu nyumbani, ila chupa ya mafuta. 3 2 Fal 3:16Akasema, Nenda, ukaazime vyombo huko nje kwa jirani zako wote, vyombo vitupu; wala usiazime vichache. 4 Kisha uingie ndani, ukajifungie mlango wewe na wanao, ukavimiminie mafuta vyombo vile vyote; navyo vilivyojaa ukavitenge. 5 Basi akamwacha, akajifungia mlango yeye na wanawe; hao wakamletea vile vyombo, na yeye akamimina. 6 Mt 14:20Ikawa, vilipokwisha kujaa vile vyombo, akamwambia mwanawe, Niletee tena chombo. Akamwambia, Hakuna tena chombo. Mafuta yakakoma. 7 Rum 13:8Ndipo akaja akamwambia yule mtu wa Mungu. Naye akasema, Nenda ukayauze mafuta haya, uilipe deni yako; nayo yaliyosalia uyatumie wewe na watoto wako.

Veja também