16 2 Sam 22:3,31;2 Nya 32:7;Zab 3:3-8;18:2;91:2;Mit 18:10;21:31;Isa 43:1;Rum 8:31Akamjibu, Usiogope; maana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao. 17 2 Fal 2:11;Zab 34:7;68:17;Zek 1:8;6:1-7;Ebr 1:14Elisha akaomba, akasema, Ee BWANA, nakusihi, mfumbue macho yake, apate kuona. BWANA akamfumbua macho yule mtumishi; naye akaona; na tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote.
Publicidade