21 Na mfalme Daudi alipoyasikia maneno hayo yote, alikasirika sana. 22 Law 19:17;Mit 10:18;1 Yoh 2:9,11;Efe 4:26,31Ila Absalomu hakusema na Amnoni wala kwa heri wala kwa shari; kwa maana Absalomu alimchukia Amnoni kwa kumlazimisha dada yake Tamari.
Absalomu ajilipiza kisasi juu ya dadaye
23 Mwa 38:12;1 Sam 25:4;2 Fal 3:4;Yos 17:18;Amu 7:24Ikawa baada ya miaka miwili mizima, Absalomu alikuwa na wenye kukata manyoya ya kondoo huko Baal-hasori uliopo upande wa Efraimu; naye Absalomu akawaalika wana wote wa mfalme.