Ushindi wa Daudi
1 2 Sam 7:9;21:15-22;1 Nya 18:1Ikawa baadaye, Daudi akawapiga Wafilisti, akawashinda; Daudi akautwaa Gathi na vijiji vyake mikononi mwa hao Wafilisti. 6 Daudi akaweka ngome katika Shamu ya Dameski, na hao Washami wakawa watumishi wa Daudi, wakaleta zawadi. Naye BWANA akampa Daudi kushinda kila alikokwenda. 13 Zab 60:1;2 Fal 14:7Basi Daudi akajipatia jina, alipokuwa akirudi, aliwaua Waedomi elfu kumi na nne katika bonde la chumvi. 14 Mwa 27:29;Hes 24:18;Zab 37:28;121:8;145:20Akaweka askari wenye kulinda ngome katika Edomu; katikati ya Edomu yote akaweka ngome, na Waedomi wote wakawa watumwa wa Daudi. Naye BWANA akampa Daudi ushindi kila kokote alikokwenda.
Wakuu wa Daudi
15 Daudi akatawala juu ya Israeli wote; naye Daudi akawafanyia hukumu na haki watu wake wote.