1 1 Tim 4:1 Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. 2 Rum 1:29 Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, 3 wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, 4 Flp 3:19 wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu; 5 Mt 7:15,21;Rum 2:20;Tit 1:16 walio na utaua kwa nje, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao. 6 Mt 23:14;Tit 1:11 Kwa maana katika hao wamo wale wajiingizao katika nyumba za watu, na kuchukua mateka wanawake wajinga wenye mizigo ya dhambi, waliochukuliwa na tamaa za kila namna; 7 2 Tim 2:25 wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli. 8 Kut 7:11,22;1 Tim 6:5;1:12 Na kama vile Yane na Yambre walivyopingana na Musa, vivyo hivyo na hawa wanapingana na ile kweli; ni watu walioharibika akili zao, wamekataliwa kwa mambo ya imani. 9 Lakini hawataendelea sana; maana upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote, kama vile na upumbavu wa hao wanaume wawili3:9 katika Kigiriki hakuna ‘wanaume wawili’. ulivyokuwa dhahiri.
10 Bali wewe umeyafuata mafundisho yangu, na mwenendo wangu, na makusudi yangu, na imani, na uvumilivu, 11 Mdo 13:14-52;14:1-20;Zab 34:19 na upendo, na subira; tena na adha zangu na mateso, mambo yaliyonipata katika Antiokia, katika Ikonio, na katika Listra, kila namna ya adha niliyoistahimili, naye Bwana aliniokoa katika hayo yote. 12 Mt 16:24;Mdo 14:22 Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa. 13 1 Tim 4:1 Lakini watu waovu na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika. 14 2 Tim 2:2 Bali wewe ukae katika mambo yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni akina nani ambao ulijifunza kwao; 15 Yn 5:39;Zab 119:99 na ya kuwa tangu utotoni umeyajua Maandiko Matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu. 16 2 Pet 1:19-21;Rum 15:4 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; 17 1 Tim 6:11 ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.