Mtu wa uvunjaji sheria
1 1 The 4:15-17Basi, ndugu, tunawasihini, kuhusu kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na kukusanyika kwetu mbele zake, 2 kwamba msifadhaishwe upesi hata kuiacha nia yenu, wala msishtushwe, kwa roho, wala kwa neno, wala kwa barua inayodhaniwa kuwa ni yetu, kana kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwapo. 3 1 Tim 4:1;Yn 17:12;1 Yoh 2:18;4:3Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yoyote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu; 4 Dan 11:36;Eze 28:2yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama cha kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.