1 Kol 4:3;1 The 5:25 Hatimaye, ndugu, tuombeeni, neno la Bwana liendelee, na kutukuzwa kote kama ilivyo kwenu; 2 na tukaokolewe kutoka kwa watu wasio haki, na waovu, maana si wote walio na imani. 3 1 The 5:24 Lakini Bwana ni mwaminifu, atakayewafanya imara na kuwalinda kutoka kwa yule mwovu. 4 1 The 4:10;Gal 5:10;2 Kor 7:16 Nasi tumemtumaini Bwana kwa mambo yenu, kwamba mnayafanya tulivyowaagiza na kwamba mtaendelea kuyafanya. 5 Bwana awaongoze mioyo yenu mkapate pendo la Mungu, na subira ya Kristo.
6 Mt 18:17;Rum 16:17;1 The 5:14;4:1 Ndugu, tunawaagiza katika jina la Bwana Yesu Kristo, jitengeni nafsi zenu kutoka kwa kila ndugu aendaye bila utaratibu, wala si kwa kufuata mapokeo mliyoyapokea kwetu. 7 1 The 2:1;1:6 Mnajua wenyewe jinsi iwapasavyo kutufuata; kwa sababu hatukuenda bila utaratibu kwenu; 8 1 Kor 4:12;Flp 3:17;1 The 2:9 wala hatukula chakula kwa mtu yeyote bure; bali kwa taabu na masumbufu, usiku na mchana tulifanya kazi, ili tusimlemee mtu wa kwenu awaye yote. 9 Mt 10:10;1 Kor 4:16;1 The 1:6,7 Si kwamba hatuna haki hiyo, ila kwa makusudi ya kuwapa mfano wa kuiga, mtufuate. 10 Mwa 3:19;1 The 3:4;4:11 Kwa kuwa hata wakati ule tulipokuwapo kwenu tuliwaagiza neno hili, kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula. 11 1 The 5:14 Maana tunasikia kwamba wako watu kwenu waendao bila utaratibu, hawana shughuli zao wenyewe, lakini wanajishughulisha na mambo ya wengine. 12 1 The 4:11 Basi tunawaagiza hao, na kuwaonya katika Bwana Yesu Kristo, wafanye kazi kwa utulivu na kula chakula chao wenyewe. 13 Gal 6:9 Lakini ninyi, ndugu, msikate tamaa katika kutenda mema. 14 1 Kor 5:9,11 Na ikiwa mtu awaye yote halishiki neno letu la barua hii, jihadharini na mtu huyo, wala msizungumze naye, apate kutahayari; 15 1 The 5:13,14 lakini msimhesabu kuwa adui, bali mwonyeni kama ndugu.
16 1 The 5:23 Sasa, Bwana wa amani mwenyewe na awape amani daima kwa njia zote. Bwana awe pamoja nanyi nyote.
17 1 Kor 16:21 Salamu zangu mimi Paulo, kwa mkono wangu mwenyewe. Hii ndiyo alama katika kila barua yangu, ndio mwandiko wangu. 18 Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi nyote.