16 Ufu 19:20Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kulia, au katika vipaji vya nyuso zao; 17 tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa awe na chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya herufi za jina lake. 18 Ufu 17:9;15:2;1 Fal 10:14;Ezr 2:13Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.
Publicidade