Mwana-kondoo na wale watu 144,000
1 Eze 9:4;Ufu 7:3;3:12Kisha nikaona, na tazama, huyo Mwana-kondoo amesimama juu ya mlima Sayuni, na watu elfu mia moja na arubaini na nne pamoja naye, wenye jina lake na jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao. 2 Eze 1:24;43:2;Ufu 1:15Nami nikasikia sauti kutoka mbinguni, kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi kuu. Na hiyo sauti niliyoisikia ilikuwa kama sauti ya wapiga vinubi, wakivipiga vinubi vyao; 3 Zab 33:3;40:3;96:1;98:1;144:9;149:1;Isa 42:10;Ufu 5:9na kuimba wimbo mpya mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele ya wale wenye uhai wanne, na wale wazee; wala hakuna mtu aliyeweza kujifunza wimbo ule, ila wale elfu mia moja na arubaini na nne, walionunuliwa katika nchi. 4 2 Kor 11:2;Efe 5:27Hawa ndio wasiojitia unajisi na wanawake, kwa maana ni bikira. Hawa ndio wamfuatao Mwana-kondoo kila aendako. Hawa wamenunuliwa katika wanadamu, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-kondoo. 5 Sef 3:13;Zab 32:2;Isa 53:9Na katika vinywa vyao haukuonekana uongo. Maana hawana mawaa.