Pular para o conteúdo
Publicidade

Ufunuo 17:1-4

SRUV Swahili Revised Union Version

Kahaba mkuu na mnyama

1 Yer 51:13;Ufu 15:1Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye yale mabakuli saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi; 2 Isa 23:17;Yer 51:7;Ufu 14:8;18:3ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wameleweshwa kwa mvinyo ya uasherati wake. 3 Ufu 13:1;Dan 7:7Akanichukua katika Roho hadi jangwani, nikaona mwanamke akiwa ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya kukufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi. 4 Yer 51:7;Eze 28:13,16Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    1 Mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na yale mabakuli saba akaja akaniambia, "Njoo, nitakuonesha adhabu ya yule kahaba mkuu, aliyeketi juu ya maji mengi. 2 Yule ambaye wafalme wa dunia walizini naye na watu walioishi duniani walilewa kwa mvinyo wa uzinzi wake."

    3 Kisha yule malaika akanichukua katika Roho wa Mungu, akanipeleka jangwani. Huko nikamwona mwanamke mmoja ameketi juu ya mnyama mwekundu aliyejaa majina ya kumkufuru Mungu mwili mzima. Mnyama huyo alikuwa na vichwa saba na pembe kumi. 4 Huyo mwanamke alikuwa amevaa mavazi ya rangi ya zambarau na nyekundu, akimetameta kwa dhahabu, vito vya thamani na lulu. Mkononi mwake alikuwa ameshika kikombe cha dhahabu kilichojaa mambo ya machukizo na uchafu wa uzinzi wake.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    1 Mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na yale mabakuli saba akaja akaniambia, "Njoo, nitakuonyesha adhabu ya yule kahaba mkuu, aketiye juu ya maji mengi. 2 Yule ambaye wafalme wa dunia walizini naye na watu wakaao duniani walilewa kwa mvinyo wa uzinzi wake."

    3 Kisha yule malaika akanichukua katika Roho akanipeleka jangwani. Huko nikamwona mwanamke mmoja ameketi juu ya mnyama mwekundu aliyejaa majina ya kumkufuru Mungu mwili mzima. Mnyama huyo alikuwa na vichwa saba na pembe kumi. 4 Huyo mwanamke alikuwa amevaa mavazi ya rangi ya zambarau na nyekundu, akimetameta kwa dhahabu, vito vya thamani na lulu. Mkononi mwake alikuwa ameshika kikombe cha dhahabu kilichojaa mambo ya machukizo na uchafu wa uzinzi wake.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.