Shangwe mbinguni
1 Zab 104:35;Ufu 11:15Baada ya hayo nikasikia sauti kama sauti ya mikutano mikubwa, sauti kubwa mbinguni, ikisema, Haleluya;19:1 Haleluya: maana yake ni, Msifuni Bwana. Wokovu na utukufu na nguvu zina Bwana Mungu wetu; 2 Kum 32:43;2 Fal 9:7;Zab 19:9;119:137;Ufu 16:7;6:10kwa kuwa hukumu zake ni za kweli na haki; maana amemhukumu yule kahaba mkuu aliyeiharibu nchi kwa uasherati wake, na kuipatiliza damu ya watumwa wake mkononi mwake. 3 Zab 104:35;Isa 34:10Wakasema mara ya pili, Haleluya. Na moshi wake hupaa juu hata milele na milele.