Wapandaji wa farasi mweupe
11 Eze 1:1;Zab 96:13;Isa 11:4;Ufu 3:14Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita. 12 Dan 10:6;Ufu 1:14;2:18;3:12Na macho yake yalikuwa kama muali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe. 13 Isa 63:1;Yn 1:1Naye amevikwa vazi lililoloweshwa katika damu, na jina lake anaitwa, Neno la Mungu. 14 Ufu 17:14Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi.