Publicidade

Apocalipse 21

Mbingu mpya na nchi mpya

1 Isa 65:17;66:22;2 Pet 3:13;Ufu 20:11Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hakuna bahari tena. 2 Isa 52:1;61:10;Ufu 3:12;19:17;Ebr 11:10Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe. 3 Eze 37:27;Law 26:11-12;Zek 2:10;Isa 8:8Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.21:3 Au hivi, Naye mwenyewe, Mungu pamoja nao, atakuwa Mungu wao.4 Isa 25:8;33:10;35:10;65:19;Ufu 7:17;Yer 31:16Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-