Pular para o conteúdo
Publicidade

Ufunuo 8:1-5

SRUV Swahili Revised Union Version

Mhuri wa saba na chetezo cha dhahabu

1 Zek 2:13;Hab 2:20Na Mwana-kondoo alipofungua mhuri wa saba, kukawa kimya mbinguni kwa muda wa kama nusu saa. 2 Mt 24:31Nami nikawaona wale malaika saba wasimamao mbele za Mungu, nao wakapewa baragumu saba. 3 Amo 9:1;Kut 30:1,3;Ufu 5:8Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhabahu, akiwa na chetezo cha dhahabu, akapewa uvumba mwingi, ili autie pamoja na maombi ya watakatifu wote juu ya madhabahu ya dhahabu, iliyo mbele ya kiti cha enzi. 4 Zab 141:2Na moshi wa ule uvumba ukapanda mbele za Mungu pamoja na maombi ya watakatifu, kutoka mkononi mwa malaika. 5 Law 16:12;Eze 10:2;Kut 19:16;Ufu 11:19;16:18Na huyo malaika akakitwaa kile chetezo, akakijaza moto wa madhabahu, akautupa juu ya nchi, kukawa radi na sauti na umeme na tetemeko la nchi.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    1 Mwana-Kondoo alipouvunja ule muhuri wa saba, pakawa kimya mbinguni kwa muda wa nusu saa.

    2 Nami nikawaona wale malaika saba wanaosimama mbele za Mungu, nao wakapewa tarumbeta saba.

    3 Malaika mwingine, aliyekuwa na chetezo cha dhahabu, akaja na kusimama mbele ya madhabahu. Akapewa uvumba mwingi ili autoe pamoja na maombi ya watakatifu wote, juu ya yale madhabahu ya dhahabu yaliyo mbele ya kile kiti cha enzi. 4 Ule moshi wa uvumba pamoja na yale maombi ya watakatifu, vikapanda juu mbele za Mungu, kutoka mkononi mwa huyo malaika. 5 Kisha yule malaika akakichukua kile chetezo, akakijaza moto kutoka kwa yale madhabahu, akautupa juu ya dunia. Pakatokea sauti za radi na ngurumo, miali ya radi na tetemeko la ardhi.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    1 Mwana-Kondoo alipoivunja ile lakiri ya saba, pakawa kimya mbinguni kwa muda wa nusu saa.

    2 Nami nikawaona wale malaika saba wanaosimama mbele za Mungu, nao wakapewa tarumbeta saba.

    3 Malaika mwingine aliyekuwa na chetezo cha dhahabu, akaja na kusimama mbele ya madhabahu. Akapewa uvumba mwingi ili autoe pamoja na maombi ya watakatifu wote, juu ya yale madhabahu ya dhahabu yaliyo mbele ya kile kiti cha enzi. 4 Ule moshi wa uvumba pamoja na yale maombi ya watakatifu, vikapanda juu mbele za Mungu, kutoka mkononi mwa huyo malaika. 5 Kisha yule malaika akachukua kile chetezo, akakijaza moto kutoka kwa yale madhabahu, akautupa juu ya dunia. Pakatokea sauti za radi, ngurumo, umeme wa radi na tetemeko la ardhi.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.