Publicidade

Atos 13

Barnaba na Sauli wateuliwa

1 Mdo 11:27Na huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, nao ni Barnaba, na Simeoni aitwaye Nigeri,13:1 ‘Nigeri’ maana yake ‘mweusi’. na Lukio Mkirene, na Manaeni aliyekuwa ndugu wa kulelewa wa mfalme Herode, na Sauli. 2 Mdo 9:15Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia. 3 Mdo 6:6;14:23;1 Tim 4:14;5:22Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-