Paulo na Sila wakiwa Beroya
10 Mara hao ndugu wakawatuma Paulo na Sila usiku hadi Beroya. Nao walipofika huko wakaingia katika sinagogi la Wayahudi. 11 Yn 5:39Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa hamu kuu, wakayachunguza Maandiko kila siku, ili waone kama mambo hayo ndivyo yalivyo. 12 Basi watu wengi miongoni mwao wakaamini, wakiwemo wanawake wa Kigiriki wenye cheo na wanaume.