Pular para o conteúdo
Publicidade

Atos 2

Kuja kwa Roho Mtakatifu

1 Law 23:15-21;Kum 16:9-11;Mdo 1:14Wakati ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja. 2 Mdo 4:31Kukaja ghafla toka mbinguni sauti kama mvumo wa upepo mkali ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. 3 Mt 3:11Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. 4 Mdo 4:31;10:44-46;19:6Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.

Veja também