Pular para o conteúdo
Publicidade

Atos 2

Petro ahutubia mkutano

14 Lakini Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti yake, akawaambia, Enyi watu wa Yudea, na ninyi nyote mkaao Yerusalemu, lijueni jambo hili, mkasikilize maneno yangu. 15 Sivyo mnavyodhani; watu hawa hawakulewa, kwa maana ni saa tatu ya mchana; 16 Yoe 2:28-32lakini jambo hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yoeli,

17 Yoe 2:28-32Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu,

nitawamwagia watu wote Roho yangu,

na wana wenu na binti zenu watatabiri;

na vijana wenu wataona maono;

na wazee wenu wataota ndoto.

18 Naam, na siku zile nitawamwagia watumishi wangu wanaume na wanawake Roho yangu,

nao watatabiri.

19 Nami nitatoa ajabu katika mbingu juu,

na ishara katika nchi chini, damu na moto,

na mvuke wa moshi.

20 Jua litageuka kuwa giza,

na mwezi kuwa damu,

kabla ya kuja ile siku ya Bwana iliyo kuu na iliyo dhahiri.

21 Rum 10:13Na itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa.

22 Yn 3:2Enyi wanaume wa Israeli, sikilizeni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua; 23 Mt 27:35;Mk 15:24;Lk 23:33;Yn 19:18;Mdo 4:28;1 Pet 1:20mtu huyu alipotolewa kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake tangu zamani, ninyi mkamsulubisha kwa mikono ya watu wabaya, mkamwua; 24 Mt 28:5-6;Mdo 3:15;Mk 16:6;Lk 24:5ambaye Mungu alimfufua, akiufungua uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao. 25 Zab 16:8-11Maana Daudi ataja habari zake,

Nilimwona Bwana mbele yangu siku zote,

Kwa kuwa yuko upande wa mkono wangu wa kulia, nisitikisike.

26 Kwa hiyo moyo wangu ukapendezewa,

ulimi wangu ukafurahi;

Tena mwili wangu nao utakaa katika matumaini.

27 Mdo 13:35Kwa maana hutaiacha roho yangu katika kuzimu;

Wala hutamtoa Mtakatifu wako aone uharibifu.

28 Umenijulisha njia za uzima;

Utanijaza furaha kwa uso wako.

29 Mdo 13:36;1 Fal 2:10Wanaume, ndugu zangu, mniwie radhi, niseme kwa ujasiri mbele yenu habari za baba yetu mkuu, Daudi, ya kuwa alifariki akazikwa, na kaburi lake liko kwetu hata leo. 30 Zab 132:11;89:3,4;2 Sam 7:12-13Basi kwa kuwa ni nabii, akijua ya kuwa Mungu amemwapia kwa kiapo, ya kwamba katika uzao wa wazawa wake atamketisha mmoja katika kiti chake cha enzi; 31 Zab 16:10yeye mwenyewe akitangulia kuyaona haya, alitaja habari za kufufuka kwake Kristo, ya kwamba roho yake haikuachwa kuzimu, wala mwili wake haukuona uharibifu. 32 Yesu huyo Mungu alimfufua, na sisi sote tu mashahidi wake. 33 Mdo 1:4Basi yeye, akiisha kupandishwa hadi mkono wa kulia wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi ya Roho Mtakatifu, amekimwaga kitu hiki mnachokiona sasa na kukisikia. 34 Zab 110:1Maana Daudi hakupanda mbinguni; bali yeye mwenyewe anasema,

Bwana alimwambia Bwana wangu,

Keti upande wa mkono wangu wa kulia.

35 Hata nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako.

36 Mdo 5:31Basi nyumba yote ya Israeli na wajue yakini ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulubisha kuwa Bwana na Kristo.

Waongofu wa Kwanza

37 Mdo 16:30Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? 38 Mdo 3:17-19;Lk 24:47Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 39 Yoe 2:32;Isa 57:19Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie. 40 Kum 32:5;Flp 2:15Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi. 41 Mdo 4:4;5:14Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapatao elfu tatu.

Veja também