44 Mdo 4:32-35Na wote walioamini walikuwa mahali pamoja, na kuwa na vitu vyote kishirika, 45 wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kulingana na haja ya kila mmoja. 46 Mdo 2:42Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe, 47 Mdo 4:4;5:14;11:21;14:1wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.
Publicidade