36 Mdo 21:5Alipokwisha kunena haya akapiga magoti, akaomba pamoja nao wote. 37 Mdo 21:6;Rum 16:16;1 Pet 5:14Wakalia sana wote, wakamwangukia Paulo shingoni, wakambusubusu, 38 Mdo 20:25wakihuzunika zaidi kwa sababu ya neno lile alilosema, ya kwamba hawatamwona uso tena. Wakamsindikiza hata merikebuni.