12 Efe 1:11,18mkimshukuru Baba, aliyewastahilisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru. 13 Kol 2:15;Lk 22:53;Efe 2:2;6:12;1:6Naye alituokoa kutoka kwa nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wake mpendwa; 14 Efe 1:7ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi.
Ukuu wa Kristo
15 Ebr 1:3;2 Kor 4:4;1 Tim 6:16;Yn 1:18Naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote. 16 Yn 1:3,10;Efe 1:10,21Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au milki, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake. 17 Mit 8:25-27;Efe 1:22Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye.