Ukuu wa Kristo
15 Ebr 1:3;2 Kor 4:4;1 Tim 6:16;Yn 1:18Naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote. 16 Yn 1:3,10;Efe 1:10,21Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au milki, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake. 17 Mit 8:25-27;Efe 1:22Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye. 18 Efe 1:22-23;4:15;5:23;Mdo 4:2;26:23;Ufu 1:5Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote. 19 Efe 1:23;Kol 2:9;Yn 1:16Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae; 20 Efe 1:7,10;2:13,16;1 Yoh 2:2na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi, au vilivyo mbinguni.