1 Efe 1:1 Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo, ndugu yetu, 2 Rum 1:7;Efe 1:2 kwa ndugu watakatifu na waaminifu katika Kristo, walioko Kolosai. Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu.
3 1 Kor 13:13;Efe 1:16;1 The 1:2,3 Twamshukuru Mungu, Baba yake Bwana wetu Yesu Kristo, siku zote tukiwaombea; 4 Efe 1:15 tangu tuliposikia habari za imani yenu katika Kristo Yesu, na upendo mlio nao kwa watakatifu wote; 5 1 Pet 1:4;Efe 1:13,18 kwa sababu ya tumaini mlilowekewa akiba mbinguni; ambalo habari zake mlizisikia zamani kwa neno la kweli ya Injili; 6 1 Tim 3:16;Efe 1:13 iliyofika kwenu, kama ilivyo katika ulimwengu wote, na kuzaa matunda na kukua, kama inavyokua kwenu pia, tangu siku mlipoisikia mkaifahamu sana neema ya Mungu katika kweli; 7 Kol 4:12;Flm 1:23 kama mlivyofundishwa na Epafra, mwenzi wetu mpendwa, aliye mhudumu mwaminifu wa Kristo kwa ajili yenu; 8 naye alitueleza upendo wenu katika Roho.
9 Efe 1:8,9,15-17;Flp 1:9 Kwa sababu hiyo sisi nasi, tangu siku ile tuliposikia, hatuachi kufanya maombi na dua kwa ajili yenu, ili mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni; 10 Efe 1:17;2:10;4:1;Flp 1:27 mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu; 11 1 Kor 1:5;Efe 1:18,19;3:16 mkiwezeshwa kwa uwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na subira ya kila namna na uvumilivu pamoja na furaha; 12 Efe 1:11,18 mkimshukuru Baba, aliyewastahilisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru. 13 Kol 2:15;Lk 22:53;Efe 2:2;6:12;1:6 Naye alituokoa kutoka kwa nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wake mpendwa; 14 Efe 1:7 ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi.
15 Ebr 1:3;2 Kor 4:4;1 Tim 6:16;Yn 1:18 Naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote. 16 Yn 1:3,10;Efe 1:10,21 Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au milki, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake. 17 Mit 8:25-27;Efe 1:22 Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye. 18 Efe 1:22-23;4:15;5:23;Mdo 4:2;26:23;Ufu 1:5 Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote. 19 Efe 1:23;Kol 2:9;Yn 1:16 Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae; 20 Efe 1:7,10;2:13,16;1 Yoh 2:2 na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi, au vilivyo mbinguni. 21 Efe 2:1,12;4:18;Rum 5:10 Na ninyi, mliokuwa hapo kwanza mmetengwa, tena adui katika nia zenu, kwa matendo yenu mabaya, amewapatanisha sasa; 22 Efe 2:11,14,16;5:27 katika mwili wa nyama yake, kwa kufa kwake, ili awalete ninyi mbele zake, watakatifu, wasio na mawaa wala lawama; 23 Mk 16:15;1 Tim 3:16;Efe 3:17;Ebr 3:14 mkidumu tu katika ile imani, hali mmewekwa juu ya msingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia habari zake, iliyohubiriwa kwa viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paulo nilikuwa mhudumu wake.
24 Efe 3:1,13 Sasa nayafurahia mateso niliyo nayo kwa ajili yenu; tena nayatimiliza katika mwili wangu yale yaliyopungua ya mateso ya Kristo, kwa ajili ya mwili wake, yaani, kanisa lake; 25 Efe 3:2,7,8 ambalo nimefanywa mhudumu wake, kulingana na uwakili wa Mungu, niliopewa kwa faida yenu, nilitimize neno la Mungu; 26 Rum 16:25,26;Efe 3:3,5,9,10 siri ile iliyofichwa tangu zamani zote na tangu vizazi vyote, bali sasa imefunuliwa kwa watakatifu wake; 27 1 Tim 1:1;Rum 16:25;Efe 3:9;1:18 ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika Mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu 28 Efe 4:13 ambaye sisi tunamhubiri habari zake tukimwonya kila mtu, na kumfundisha kila mtu katika hekima yote, tupate kumleta kila mtu mtimilifu katika Kristo. 29 Flp 4:13;Efe 3:7,20 Nami najitaabisha kwa neno lilo hilo, nikijitahidi kwa kadiri ya kutenda kazi kwake atendaye kazi ndani yangu kwa nguvu.