9 Efe 4:22Msiambiane uongo, kwa kuwa mmevua kabisa utu wa kale, pamoja na matendo yake; 10 Mwa 1:26;Efe 4:24mkivaa utu mpya, unaofanywa upya katika ufahamu kulingana na mfano wake yeye aliyeuumba. 11 Gal 3:28Hapo hapana Mgiriki wala Myahudi, kutahiriwa wala kutotahiriwa, mgeni wala mshenzi, mtumwa wala muungwana, bali Kristo ni yote, na katika yote.
Publicidade