Publicidade

Daniel 12

Kufufuka kwa wafu

1 Ufu 16:18;Isa 11:11;Yer 30:7;Hos 3:5;Yoe 3:16;Rum 11:26;Kut 32:32;Isa 4:3;Eze 13:9;Lk 10:20;Mt 24:21;Mk 13:19;Ufu 7:14;12:7Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako; na kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati huo huo; na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile. 2 Isa 26:19;Mt 25:46;Yn 5:29Tena, wengi wa hao wanaolala katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele. 3 1 Kor 15:41Na walio na hekima watang’aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang’aa kama nyota milele na milele.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-