10 Zab 37:35,36;Eze 31:3;Isa 10:33,34Njozi za kichwa changu kitandani mwangu zilikuwa hivi; niliona, na tazama, palikuwa na mti katikati ya nchi, urefu wake mkubwa sana. 11 Mti ule ukakua, ukawa na nguvu, urefu wake ulifika mpaka mbinguni, na kuonekana kwake mpaka mwisho wa dunia. 12 Eze 17:23;Omb 4:20Majani yake yalikuwa mazuri, na matunda yake mengi, na ndani yake chakula cha kuwatosha watu wote; wanyama wa mwituni walipata uvuli chini yake, na ndege wa angani walikaa katika matawi yake; kila kitu chenye mwili kilipata chakula kwake.
20 Ule mti uliouona, uliokua, ukawa na nguvu, urefu wake ukafika mpaka mbinguni, na kuonekana kwake mpaka dunia yote; 21 ambao majani yake yalikuwa mazuri, na matunda yake mengi, na ndani yake chakula cha kuwatosha wote; ambao chini yake wanyama wa mwituni walikaa, na ndege wa angani walikuwa na makao yao katika matawi yake; 22 Ayu 20:5;Dan 2:38;Yer 27:6-8ni wewe, Ee mfalme, uliyekua, na kupata nguvu; maana ukuu wako umekua na kufika mpaka mbinguni, na mamlaka yako yamefika mpaka mwisho wa dunia.