4 Zab 104:5;2 Pet 3:10Kizazi huenda, kizazi huja; nayo dunia hudumu daima. 5 Zab 19:5Jua lachomoza, na jua lashuka, na kufanya haraka kwenda mahali pa maawio yake. 6 Yn 3:8Upepo huvuma kuelekea kusini, kisha huvuma kuelekea kaskazini; hugeuka daima katika mwendo wake, nao huyarudia mazunguko yake. 7 Ayu 38:10;Zab 104:8Mito yote huingia baharini, lakini bahari haijai; huko iendako mito, ndiko irudiko tena.
Publicidade