Pular para o conteúdo
Publicidade

Mhubiri 2:13-16

SRUV Swahili Revised Union Version

13 Ndipo nilipoona ya kuwa kweli hekima hupita upumbavu, kwa kadiri nuru ipitavyo giza; 14 Mhu 8:1;9:2macho yake mwenye hekima yamo kichwani mwake, lakini mpumbavu huenda gizani; ila hata hivyo nikatambua ya kwamba ni tukio moja la mwisho liwapatalo wote sawasawa. 15 Nikasema moyoni mwangu, Kama limpatavyo mpumbavu, ndivyo litakavyonipata mimi nami; basi, kwa nini nikawa na hekima zaidi? Nikasema moyoni mwangu ya kuwa hayo nayo ni ubatili. 16 Maana hakuna kumbukumbu la milele la mwenye hekima, wala la mpumbavu; kwa sababu siku zijazo wote pia watakuwa wamekwisha kusahauliwa. Na mwenye hekima, jinsi gani anavyokufa sawasawa na mpumbavu!

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    13 Nikaona kuwa hekima ni bora kuliko upumbavu,

    kama vile nuru ilivyo bora kuliko giza.

    14 Mtu mwenye hekima ana macho katika kichwa chake,

    lakini mpumbavu anatembea gizani;

    lakini nikaja kuona kwamba

    wote wawili hatima yao inafanana.

    15 Kisha nikafikiri moyoni mwangu,

    "Hatima ya mpumbavu itanipata mimi pia.

    Nitafaidi nini basi kwa kuwa na hekima?"

    Nikasema moyoni mwangu,

    "Hili nalo ni ubatili."

    16 Kwa maana kwa mtu mwenye hekima,

    kama ilivyo kwa mpumbavu,

    hatakumbukwa kwa muda mrefu,

    katika siku zijazo wote watasahaulika.

    Kama vile ilivyo kwa mpumbavu,

    mtu mwenye hekima pia lazima atakufa!

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    13 Nikaona kuwa hekima ni bora kuliko upumbavu,

    kama vile nuru ilivyo bora kuliko giza.

    14 Mtu mwenye hekima ana macho katika kichwa chake,

    lakini mpumbavu anatembea gizani;

    lakini nikaja kuona kwamba

    wote wawili hatima yao inafanana.

    15 Kisha nikafikiri moyoni mwangu,

    "Hatima ya mpumbavu itanipata mimi pia.

    Nitafaidi nini basi kwa kuwa na hekima?"

    Nikasema moyoni mwangu,

    "Hili nalo ni ubatili."

    16 Kwa maana kwa mtu mwenye hekima,

    kama ilivyo kwa mpumbavu,

    hatakumbukwa kwa muda mrefu,

    katika siku zijazo wote watasahaulika.

    Kama vile ilivyo kwa mpumbavu,

    mtu mwenye hekima pia lazima atakufa!

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.