9 Neh 2:8Maana alianza kukwea kutoka Babeli siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, naye akafika Yerusalemu siku ya kwanza ya mwezi wa tano, kama mkono mwema wa Mungu wake ulivyokuwa pamoja naye. 10 1 Sam 7:3;2 Nya 12:14;Zab 10:18;119:45;Kum 33:10;Neh 8:1;Mal 2:7;2 Tim 4:2Kwa maana huyo Ezra alikuwa ameuelekeza moyo wake kuitafuta sheria ya BWANA, na kuitenda, na kufundisha maagizo na hukumu katika Israeli.