Watu wafunga na kuomba amani
21 2 Nya 20:3;Law 16:29;Isa 58:3,5;Zab 5:8Ndipo nikaamuru kufunga, hapo penye mto Ahava, ili tupate kujinyenyekeza mbele za Mungu, na kutafuta kwake njia iliyonyoka, kwa ajili yetu sisi wenyewe, na kwa ajili ya watoto wetu, na kwa mali yetu yote. 22 1 Kor 9:15;1 Nya 28:9;Ezr 7:6,9;Zab 33:18,19;Isa 3:10;Rum 8:28;1 Pet 3:12;Zab 34:16;2 Nya 15:2Maana niliona haya kumwomba mfalme kikosi cha askari na wapanda farasi, ili kutusaidia juu ya adui njiani; kwa maana tulikuwa tumesema na mfalme, tukinena, Mkono wa Mungu u juu ya watu wote wamtafutao, kuwatendea mema; bali uweza wake na ghadhabu yake ni juu ya wote wamkataao. 23 Kum 4:29;1 Nya 5:20;2 Nya 33:13;Isa 19:22;Yer 29:12,13Basi tukafunga, tukamsihi Mungu wetu kwa ajili ya hayo; naye akatutakabali.