Kutoka mauti hadi uhai
1 Kol 1:21;2:13Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; 2 Efe 6:12;Tit 3:3;Yn 12:31;Kol 1:13ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi; 3 Kol 3:6ambao zamani, sisi sote nasi tulienda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira, kama wengineo wote. 4 Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; 5 Lk 15:24,32;Efe 5:14;Rum 6:13hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alitufanya kuwa hai pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema.