16 Efe 1:7;6:10;Kol 1:11awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake katika utu wa ndani. 17 Yn 14:23;Kol 1:23;2:7Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo; 18 Kol 2:2ili mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina; 19 Kol 2:3na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu.