Pular para o conteúdo
Publicidade

Efésios 4

Amri za maisha mapya

25 Zek 8:16;Kol 3:8Basi uvueni uongo, mkaseme kweli kila mtu na jirani yake; kwa maana tu viungo, kila mmoja kiungo cha wenzake. 26 Zab 4:4;Yak 1:19,20Muwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka; 27 wala msimpe Ibilisi nafasi. 28 1 The 4:11Mwizi asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akifanya kazi iliyo nzuri kwa mikono yake mwenyewe, apate kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji. 29 Efe 5:4;Kol 3:16,17;4:6Neno lolote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia. 30 Efe 1:13;Isa 63:10Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa mhuri hata siku ya ukombozi. 31 Kol 1:5Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matusi yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya; 32 Kol 3:13;Mt 6:14;18:22-35tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.

Veja também