Pular para o conteúdo
Publicidade

Waefeso 5:21,22,25,28,29

SRUV Swahili Revised Union Version

Nyumba ya Kikristo

21 1 Pet 5:5Hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo.

22 Kol 3:18;1 Pet 3:1;Mwa 3:16Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu.

25 Kol 3:19;1 Pet 3:7Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda kanisa, akajitoa kwa ajili yake; 28 Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. 29 Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake popote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea kanisa.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    21 Nyenyekeaneni ninyi kwa ninyi kutokana na kumcha Al-Masihi.

    22 Ninyi wake, watiini waume zenu kama vile mnavyomtii Bwana Isa.

    25 Ninyi waume, wapendeni wake zenu, kama vile Al-Masihi alivyoipenda jumuiya ya waumini na akajitoa kwa ajili yake, 28 Vivyo hivyo imewapasa waume kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. 29 Hakuna mtu anayeuchukia mwili wake mwenyewe, bali huulisha na kuutunza vizuri, kama Al-Masihi anavyoitunza jumuiya yake ya waumini.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    21 Nyenyekeaneni ninyi kwa ninyi kwa heshima kwa ajili ya Kristo.

    22 Ninyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana.

    25 Ninyi waume, wapendeni wake zenu, kama vile Kristo alivyolipenda Kanisa akajitoa kwa ajili yake 28 Vivyo hivyo imewapasa waume kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. 29 Hakuna mtu anayeuchukia mwili wake mwenyewe, bali huulisha na kuutunza vizuri, kama Kristo anavyolitunza Kanisa lake.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.