Watoto na wazazi
1 Kol 3:20Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki. 2 Kut 20:12;Kum 5:16Waheshimu baba yako na mama yako; hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, 3 Upate heri na kuishi siku nyingi katika dunia. 4 Kol 3:21;Isa 50:5;Mit 2:2;3:11;19:18;Kum 6:7,20-25;Zab 78:4Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maagizo ya Bwana.