13 1 Fal 20:11Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. 14 Isa 11:5;59:17;Lk 12:35;1 Pet 1:13;1 The 5:8Basi simameni, mkiwa mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, 15 Isa 52:7;40:3,9na kama viatu vilivyofungiwa miguuni mwenu muwe tayari kutangaza Injili ya amani; 16 1 Pet 5:9;1 Yoh 5:4zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. 17 Isa 59:17;11:4;49:2;51:16;1 The 5:8;Hos 6:5Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; 18 Mt 26:41;Kol 4:2,3kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;