12 1 Pet 1:17;Zab 2:11Basi, wapendwa wangu, kama vile mlivyotii sikuzote, si wakati mimi nilipokuwapo tu, bali sasa zaidi sana mimi nisipokuwapo, utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka. 13 Yn 15:5;2 Kor 3:5;1 The 2:13Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.
14 1 Pet 4:9Yatendeni mambo yote pasipo manung’uniko wala mashindano, 15 Kum 32:5;Mt 5:14;10:16;Flp 1:10;Efe 5:8;Kum 32:5;Mdo 2:40mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu, 16 1 The 2:19;Gal 2:2;Isa 49:4;65:23mkishika neno la uzima; nipate sababu ya kuona fahari katika siku ya Kristo, ya kuwa sikupiga mbio bure wala sikujitaabisha bure.