26 Yn 1:12;Rum 8:17Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu. 27 Rum 6:3;13:14Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo. 28 Rum 10:12;1 Kor 12:13Hakuna Myahudi wala Mgiriki. Hakuna mtumwa wala huru. Hakuna mwanamume wala mwanamke. Maana ninyi nyote mmekuwa wamoja katika Kristo Yesu.