Kazi za kimwili
16 Basi nasema, Nendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. 17 Rum 7:15-23;Yak 4:5;1 Pet 2:11Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.