Kazi za kimwili
16 Basi nasema, Nendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. 17 Rum 7:15-23;Yak 4:5;1 Pet 2:11Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.
Tunda la Roho
22 Efe 5:9Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, 23 1 Tim 1:9upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. 24 Rum 6:6;Kol 3:5;1 Pet 2:11Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. 25 Rum 8:4Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.