1 Mt 18:15;Yak 5:19 Ndugu zangu, mtu akishikwa katika kosa lolote, ninyi mlio wa Roho mrejesheni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe. 2 Mchukuliane mizigo na hivyo kuitimiza sheria ya Kristo. 3 Maana mtu akijiona kuwa ni kitu, naye si kitu, ajidanganya nafsi yake. 4 2 Kor 13:5 Lakini kila mtu na aipime kazi yake mwenyewe, ndipo atakapokuwa na sababu ya kujisifu ndani ya nafsi yake tu, wala si kwa mwenzake. 5 Rum 14:12 Maana kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe.
6 1 Kor 9:14 Mwanafunzi na amshirikishe mwalimu wake katika mema yote. 7 Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa chochote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. 8 Rum 8:13;Yn 6:63;3:6 Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele. 9 2 The 3:13 Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho. 10 2 Pet 1:7 Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.
11 Tazameni niandikavyo kwa herufi kubwa niwaandikiapo kwa mkono wangu mimi mwenyewe! 12 Gal 5:11;Flp 3:18 Wote watakao kuonekana ni wazuri kwa mambo ya mwili, ndio wanaowashurutisha kutahiriwa; makusudi wasiudhiwe kwa ajili ya msalaba wa Kristo, hilo tu. 13 Kwa maana hata wao wenyewe waliotahiriwa hawaishiki sheria; bali wanataka ninyi mtahiriwe, wapate kuona fahari katika miili yenu. 14 1 Kor 1:31;2:2 Lakini mimi, la hasha, nisione fahari juu ya kitu chochote ila msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambao kwa huo ulimwengu umesulubishwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu. 15 Gal 5:6;1 Kor 7:19 Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutotahiriwa, ila kiumbe kipya. 16 Zab 125:5;128:6;Flp 3:3 Na wote watakaoenenda kwa kanuni hiyo, amani na iwe kwao na rehema, naam, kwa Israeli wa Mungu.
17 2 Kor 4:10 Tangu sasa mtu asinitaabishe; kwa maana ninachukua mwilini mwangu chapa zake Yesu.
18 Ndugu zangu, neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja na roho zenu. Amina.