Pular para o conteúdo
Publicidade

Mwanzo 12:1,4,10-13

SRUV Swahili Revised Union Version

Abramu aitwa na Mungu

1 Mdo 7:2-3;Ebr 11:8;Mwa 15:7BWANA akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonesha; 4 Basi Abramu akaenda, kama BWANA alivyomwamuru; Lutu akaenda pamoja naye. Naye Abramu alikuwa mtu wa miaka sabini na mitano alipotoka Harani.

Abramu na Sarai nchini Misri

10 Mwa 26:1;Zab 105:13;Mwa 43:1Basi kulikuwa na njaa katika nchi ile; Abramu akashuka Misri, akae huko kwa muda maana njaa ilikuwa kali katika nchi. 11 Mwa 26:7Ikawa alipokuwa karibu kuingia Misri, akamwambia Sarai mkewe, Tazama, najua ya kuwa u mwanamke mzuri wa uso; 12 Mwa 20:11basi itakuwa, Wamisri watakapokuona watasema, Huyu ni mkewe; kisha wataniua mimi na wewe watakuacha hai. 13 Mwa 20:2;26:7;Zab 25:21;Efe 4:25Tafadhali useme, wewe u ndugu yangu, iwe heri kwangu kwa ajili yako, na nafsi yangu iishi kwa ajili yako.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    1 Mwenyezi Mungu alikuwa amemwambia Abramu, "Ondoka katika nchi yako, uache jamii yako na nyumba ya baba yako, uende hadi nchi nitakayokuonesha.

    4 Hivyo Abramu akaondoka kama Mwenyezi Mungu alivyokuwa amemwambia; naye Lutu akaondoka pamoja naye. Abramu alipoitwa aondoke Harani, alikuwa na umri wa miaka sabini na tano.

    10 Basi kulikuwa na njaa katika nchi hiyo, naye Abramu akashuka kwenda Misri kukaa huko kwa muda, kwa maana njaa ilikuwa kali. 11 Alipokaribia kuingia Misri, akamwambia Sarai mkewe, "Ninajua kwamba wewe ni mwanamke mzuri wa sura. 12 Wamisri watakapokuona, watasema, ‘Huyu ni mke wake.’ Kisha wataniua, lakini wewe watakuacha hai. 13 Sema wewe ni dada yangu, ili nitendewe mema kwa ajili yako, na maisha yangu yahifadhiwe kwa sababu yako."

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    1 Bwana akawa amemwambia Abramu, "Ondoka kutoka nchi yako, uache jamii yako na nyumba ya baba yako, uende hadi nchi nitakayokuonyesha.

    4 Hivyo Abramu akaondoka kama Bwana alivyokuwa amemwambia; naye Loti akaondoka pamoja naye. Wakati Abramu alipoitwa aondoke Harani, alikuwa na miaka sabini na mitano.

    10 Basi kulikuwako na njaa katika nchi, naye Abramu akashuka kwenda Misri kukaa huko kwa muda, kwa maana njaa ilikuwa kali. 11 Alipokuwa karibu kuingia Misri, akamwambia Sarai mkewe, "Ninajua ya kwamba wewe ni mwanamke mzuri wa sura. 12 Wakati Wamisri watakapokuona, watasema, ‘Huyu ni mke wake.’ Ndipo wataniua, lakini wewe watakuacha hai. 13 Sema wewe ni dada yangu, ili nitendewe mema kwa ajili yako, na maisha yangu yatahifadhiwa kwa sababu yako."

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.