Pular para o conteúdo
Publicidade

Mwanzo 12:1-4

SRUV Swahili Revised Union Version

Abramu aitwa na Mungu

1 Mdo 7:2-3;Ebr 11:8;Mwa 15:7BWANA akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonesha; 2 Mwa 17:6;18:18;46:3;Hes 23:10;Kum 26:5;1 Fal 3:8nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka; 3 Gal 3:8;Mwa 24:35;27:29;Kut 23:22;Hes 24:9;Mwa 22:18;26:4;28:14;Zab 72:17;Mdo 3:25nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa. 4 Basi Abramu akaenda, kama BWANA alivyomwamuru; Lutu akaenda pamoja naye. Naye Abramu alikuwa mtu wa miaka sabini na mitano alipotoka Harani.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    1 Mwenyezi Mungu alikuwa amemwambia Abramu, "Ondoka katika nchi yako, uache jamii yako na nyumba ya baba yako, uende hadi nchi nitakayokuonesha.

    2 "Nitakufanya taifa kubwa

    na nitakubariki,

    Nitalikuza jina lako,

    nawe utakuwa baraka.

    3 Nitawabariki wale wanaokubariki,

    na yeyote akulaaniye nitamlaani;

    na kupitia kwako mataifa yote duniani

    yatabarikiwa."

    4 Hivyo Abramu akaondoka kama Mwenyezi Mungu alivyokuwa amemwambia; naye Lutu akaondoka pamoja naye. Abramu alipoitwa aondoke Harani, alikuwa na umri wa miaka sabini na tano.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    1 Bwana akawa amemwambia Abramu, "Ondoka kutoka nchi yako, uache jamii yako na nyumba ya baba yako, uende hadi nchi nitakayokuonyesha.

    2 "Mimi nitakufanya taifa kubwa

    na nitakubariki,

    Nitalikuza jina lako,

    nawe utakuwa baraka.

    3 Nitawabariki wale wanaokubariki,

    na yeyote akulaaniye nitamlaani;

    na kupitia kwako mataifa yote duniani

    yatabarikiwa."

    4 Hivyo Abramu akaondoka kama Bwana alivyokuwa amemwambia; naye Loti akaondoka pamoja naye. Wakati Abramu alipoitwa aondoke Harani, alikuwa na miaka sabini na mitano.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.