3 Kut 3:6Abramu akaanguka kifudifudi. Mungu akamwambia, 4 Hili ndilo agano langu nawe, utakuwa baba wa mataifa mengi, 5 Rum 4:17wala jina lako hutaitwa tena Abramu, lakini jina lako litakuwa Abrahamu,17:5 Abrahamu: Abrahamu kwa maana ya ‘baba wa wengi’. kwani nimekuweka uwe baba wa mataifa mengi. 6 Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, nami nitakufanya kuwa mataifa, na wafalme watatoka kwako. 7 Lk 1:55;Mwa 26:24;28:13;Ebr 11:16;Rum 9:7-9Agano langu nitalifanya imara kati yangu na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako. 8 Mdo 7:5;Kut 6:7;29:45;Law 26:12;Kum 4:37;14:2;26:18;Zab 48:14;Ufu 21:7Nami nitakupa wewe na uzao wako baada yako nchi hii unayokaa kama mgeni, nchi yote ya Kanaani, kuwa milki ya milele; nami nitakuwa Mungu wao.
9 Zab 25:10Mungu akamwambia Abrahamu, Nawe ulishike agano langu, wewe, uzao wako na vizazi vyao. 10 Mdo 7:8;Rum 4:11Hili ndilo agano langu utakalolishika, kati yangu nawe, na uzao wako, Kila mwanamume wa kwenu atatahiriwa. 11 Mdo 7:8;Rum 4:11;Gal 6:15Mtatahiriwa nyama ya magovi yenu, na jambo hilo litakuwa ishara ya agano kati ya mimi na ninyi.