Pular para o conteúdo
Publicidade

Mwanzo 20:2,9-13

SRUV Swahili Revised Union Version

2 Mwa 12:11-15;26:7Abrahamu akanena juu ya Sara mkewe, "Huyu ni dada yangu". Basi Abimeleki mfalme wa Gerari akatuma watu wakamtwaa Sara. 9 Mwa 39:9;Yos 7:25Kisha Abimeleki akamwita Abrahamu, akamwambia, Umetutenda nini? Nimekukosa nini, hata ukaleta juu yangu na juu ya ufalme wangu dhambi kuu? Umenitenda matendo yasiyotendeka. 10 Abimeleki akamwambia Abrahamu, Umeona nini hata ukatenda jambo hili? 11 Mwa 42:18;Neh 5:15;Mit 16:6Abrahamu akasema, Kwa kuwa niliona, hakika hapana hofu ya Mungu mahali hapa, nao wataniua kwa ajili ya mke wangu. 12 Mwa 11:29Hata hivyo, kwa kweli yeye ni dada yangu, yaani binti wa baba yangu na wala sio binti wa mama yangu; ndipo akawa mke wangu. 13 Mwa 12:1,9,10,13Ikawa hapo Mungu aliponisafirisha kutoka nyumba ya baba yangu, nikamwambia, Hii ndiyo fadhili yako, utakayonifanyia. Kila mahali tuingiapo, useme, Huyu ni kaka yangu.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    2 Huko Ibrahimu akasema kuhusu Sara mkewe, "Huyu ni dada yangu." Kisha Abimeleki mfalme wa Gerari akaagiza Sara aletwe, naye akamchukua awe mkewe.

    9 Kisha Abimeleki akamwita Ibrahimu na kumwambia, "Wewe umetufanyia nini? Nimekukosea nini hata ukaleta hatia kubwa namna hii kwangu na kwa ufalme wangu? Umenifanyia mambo ambayo hayakupasa kufanyika." 10 Abimeleki akamuuliza Ibrahimu, "Ulikuwa na kusudi gani kufanya hivi?"

    11 Ibrahimu akajibu, "Niliwaza kwamba, ‘Hakika hakuna hofu ya Mungu mahali hapa, nao wataniua kwa sababu ya mke wangu.’ 12 Pamoja na hayo, ni kweli kwamba yeye ni dada yangu, binti ya baba yangu ingawa si mtoto wa mama yangu; basi akawa mke wangu. 13 Mungu aliponifanya nisafiri mbali na nyumbani mwa baba yangu, nilimwambia, ‘Hivi ndivyo utakavyoonesha pendo lako kwangu: Kila mahali tutakapoenda, sema hivi kunihusu, "Huyu ni kaka yangu." ’ "

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    2 huko Abrahamu akasema kuhusu Sara mkewe, "Huyu ni dada yangu." Kisha Abimeleki mfalme wa Gerari akatuma Sara aletwe, naye akamchukua.

    9 Kisha Abimeleki akamwita Abrahamu na kumwambia, "Wewe umetufanyia nini? Nimekukosea nini hata ukaleta hatia kubwa namna hii juu yangu na ufalme wangu? Umenifanyia mambo ambayo hayakupasa kufanyika." 10 Abimeleki akamuuliza Abrahamu, "Ulikuwa na kusudi gani kufanya hivi?"

    11 Abrahamu akajibu, "Niliwaza kwamba, ‘Hakika hakuna hofu ya Mungu mahali hapa, nao wataniua kwa sababu ya mke wangu.’ 12 Pamoja na hayo, ni kweli kwamba yeye ni dada yangu, binti wa baba yangu ingawa si mtoto wa mama yangu; basi akawa mke wangu. 13 Wakati Bwana aliponifanya nisafiri mbali na nyumbani mwa baba yangu, nilimwambia, ‘Hivi ndivyo utakavyoonyesha pendo lako kwangu: Kila mahali tutakapokwenda, kuhusu mimi sema, "Huyu ni kaka yangu." ’ "

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.