3 Zab 105:14;Ayu 4:12;33:15;Mwa 19:7Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto ya usiku, akamwambia, Umekuwa mfu wewe kwa sababu ya mwanamke huyu uliyemtwaa, maana ni mke wa mtu. 4 Mwa 18:23-25Basi Abimeleki alikuwa hakumkaribia, akasema, Ee Bwana, Je! Utaua hata taifa lenye haki? 5 Je! Hukuniambia mwenyewe, "Huyu ni dada yangu?" Na mwanamke mwenyewe naye akasema, "Huyu ni kaka yangu". Kwa ukamilifu wa moyo wangu, na kwa kutojua kwangu, nimefanya hivi. 6 Mwa 35:5;Kut 34:4;1 Sam 25:26,34Mungu akamwambia katika ndoto, Nami nimejua ya kwamba kwa ukamilifu wa moyo wako umefanya hivi, ndipo nami nikakuzuia usinitendee dhambi, kwa hiyo sikukuacha umguse. 7 1 Sam 7:5;2 Fal 5:11;Ayu 42:8;Yak 5:14-16;1 Yoh 5:16Basi sasa umrudishe mwanamke kwa mtu huyo, maana yeye ni nabii, naye atakuombea, upate kuishi. Bali usipomrudisha, fahamu ya kwamba kwa hakika utakufa wewe na watu wote ulio nao.
Mwanzo 20:3-7
Em outras traduções
- ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas
3 Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto usiku na kumwambia, "Wewe ni kama mfu kwa sababu ya huyu mwanamke uliyemchukua; yeye ni mke wa mtu."
4 Wakati huo Abimeleki alikuwa bado hajamsogelea, kwa hiyo akasema, "Je, Bwana utaliharibu taifa lisilo na hatia? 5 Hakusema kwangu, ‘Huyu ni dada yangu’; naye Sara pia hakusema, ‘Huyu ni kaka yangu’? Nimefanya haya kwa dhamiri safi na mikono safi."
6 Kisha Mungu akamwambia katika ndoto ile, "Ndiyo, najua kwamba umefanya haya kwa dhamiri safi, kwa hiyo nimekuzuia usinitende dhambi. Ndiyo sababu sikukuacha umguse. 7 Sasa umrudishe huyo mke wa mtu, kwa maana ni nabii, naye atakuombea nawe utaishi. Lakini kama hutamrudisha, ujue kwa hakika kuwa wewe na watu wako wote mtakufa."
- ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli
3 Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto wakati wa usiku na kumwambia, "Wewe ni kama mfu kwa sababu ya huyu mwanamke uliyemchukua; yeye ni mke wa mtu."
4 Wakati huo Abimeleki alikuwa bado hajamsogelea, kwa hiyo akasema, "Je, Bwana utaliharibu taifa lisilo na hatia? 5 Hakusema kwangu, ‘Huyu ni dada yangu,’ naye Sara pia hakusema, ‘Huyu ni kaka yangu’? Nimefanya haya kwa dhamiri njema na mikono safi."
6 Kisha Mungu akamwambia katika ndoto, "Ndiyo, najua ya kwamba umefanya haya kwa dhamiri safi, kwa hiyo nimekuzuia usinitende dhambi. Ndiyo sababu sikukuacha umguse. 7 Sasa umrudishe huyo mke wa mtu, kwa maana ni nabii, naye atakuombea nawe utaishi. Lakini kama hutamrudisha, ujue kwa hakika kuwa wewe na watu wako wote mtakufa."
Direitos das traduções citadas
Estes versículos te tocaram? Ore agora!
+581 estão orando agora.
Junte-se à corrente de oração.