Pular para o conteúdo
Publicidade

Mwanzo 21:1,2,6,7

SRUV Swahili Revised Union Version

Kuzaliwa kwa Isaka

1 1 Sam 2:21;Mwa 17:19;18:10;Gal 4:23BWANA akamjia Sara kama alivyonena, na BWANA akamfanyia kama alivyosema. 2 Ebr 11:11;Mdo 7:8Sara akapata mimba akamzalia Abrahamu mwana wa kiume katika uzee wake, kwa muhula alioambiwa na Mungu. 6 Zab 126:2;Isa 54:1;Lk 1:14,58Sara akasema, Mungu amenifanyia kicheko; kila asikiaye atacheka pamoja nami. 7 Mwa 18:11Akasema, Ni nani angemwambia Abrahamu, Sara atanyonyesha wana? Maana nimemzalia mwana katika uzee wake.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    1 Wakati huu Mwenyezi Mungu akamrehemu Sara kama alivyokuwa amesema, na Mwenyezi Mungu akamtendea Sara kama alivyoahidi. 2 Sara akapata mimba, na akamzalia Ibrahimu mwana katika uzee wake, katika majira yale Mungu alikuwa amemwahidi.

    6 Sara akasema, "Mungu ameniletea kicheko, na kila mmoja atakayesikia jambo hili atacheka pamoja nami." 7 Akaongeza kusema, "Nani angemwambia Ibrahimu kuwa Sara angenyonyesha watoto? Lakini nimemzalia mwana katika uzee wake."

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    1 Wakati huu Bwana akamrehemu Sara kama alivyokuwa amesema, naye Bwana akamtendea Sara kile alichokuwa ameahidi. 2 Sara akapata mimba, akamzalia Abrahamu mwana katika uzee wake, majira yale ya Mungu aliomwahidi.

    6 Sara akasema, "Mungu ameniletea kicheko, kila mmoja atakayesikia jambo hili atacheka pamoja nami." 7 Akaongeza kusema, "Nani angemwambia Abrahamu kuwa Sara angenyonyesha watoto? Tena nimemzalia mwana katika uzee wake."

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.