16 Ebr 6:13-14;Zab 105:9;Lk 1:73akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema BWANA, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee, 17 Ebr 11:12;Mwa 15:5;Yer 33:22;Mwa 13:16;24:60;Mik 1:9katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki lango la adui zao; 18 Mdo 3:25;Mwa 12:3;18:18;Gal 3:8,9,16,18;Mwa 22:3,10;26:5na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu.