Yakobo akwepa ghadhabu ya Esau
41 Mwa 37:4;50:3;Oba 1:10;1 Yoh 3:12Esau akamchukia Yakobo kwa ajili ya ile baraka babaye aliyombariki. Esau akasema moyoni mwake, Siku za kumlilia baba yangu zinakaribia, ndipo nitakapomwua ndugu yangu Yakobo. 42 Zab 64:5Rebeka akaarifiwa maneno ya Esau, mwanawe mkubwa. Akatuma mtu kumwita Yakobo, mwanawe mdogo, akamwambia, Tazama, katika habari zake Esau, ndugu yako, anajifariji moyo wake, maana anakusudia kukuua. 43 Mwa 11:31Na sasa, mwanangu, sikia sauti yangu, uondoke, ukimbilie kwa Labani, ndugu yangu huko Harani; 44 ukae kwake siku chache, hadi ghadhabu ya ndugu yako iishe; 45 hadi ikuondokee ghadhabu ya ndugu yako, akasahau uliyomtenda. Ndipo nitakapotuma watu kukuchukua kutoka huko. Kwa nini nifiwe nanyi nyote wawili siku moja?