Pular para o conteúdo
Publicidade

Mwanzo 3:6,8,15,19,24

SRUV Swahili Revised Union Version

6 Rum 5:12-19Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alichuma matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala. 8 Ayu 31:33;38:1;Zab 139:1-12;Yer 23:34;Amo 9:3Kisha wakasikia sauti ya BWANA Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, BWANA Mungu asiwaone. 15 Hes 21:6,7;Rum 16:20;Ebr 2:14;1 Yoh 3:8;Ufu 12:17nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino. 19 1 Kor 15:21,22kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.

24 Mwa 2:8;Zab 104:4;Ebr 1:7;Yn 14:6Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huku na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    6 Mwanamke alipotambua kwamba tunda la mti huo lilikuwa zuri kwa chakula na la kupendeza macho, tena linatamanika kwa kujipatia hekima, basi akachuma matunda yake, akala. Pia akampa mumewe, aliyekuwa pamoja naye, akala.

    8 Yule mwanaume na mkewe waliposikia sauti ya Bwana Mwenyezi Mungu akitembea bustanini jioni, wakajificha kutoka kwa Bwana Mwenyezi Mungu katikati ya miti ya bustani.

    15 Nami nitaweka uadui

    kati yako na huyu mwanamke,

    na kati ya uzao wako na wake;

    yeye atakuponda kichwa,

    nawe utamuuma kisigino."

    19 Kwa jasho la uso wako

    utakula chakula chako

    hadi utakaporudi ardhini,

    kwa kuwa ulitwaliwa kutoka humo;

    wewe u mavumbi

    na mavumbini utarudi."

    24 Baada ya kumfukuzia mbali Adamu, Mungu akaweka makerubi mashariki mwa Bustani ya Edeni, pamoja na upanga wa moto ukimulika kila upande kulinda njia ya kuuendea mti wa uzima.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    6 Mwanamke alipoona ya kuwa tunda la mti huo lilikuwa zuri kwa chakula na la kupendeza macho, tena linatamanika kwa kujipatia hekima, basi akachuma katika matunda yake, akala, pia akampa mumewe, aliyekuwa pamoja naye, naye akala.

    8 Ndipo yule mwanaume na mkewe, waliposikia sauti ya Bwana Mungu alipokuwa akitembea bustanini jioni, wakajificha kutoka mbele za Bwana Mungu katikati ya miti ya bustani.

    15 Nami nitaweka uadui

    kati yako na huyo mwanamke,

    na kati ya uzao wako na wake,

    yeye atakuponda kichwa,

    nawe utamuuma kisigino."

    19 Kwa jasho la uso wako

    utakula chakula chako

    hadi utakaporudi ardhini,

    kwa kuwa ulitwaliwa kutoka humo,

    kwa kuwa wewe u mavumbi

    na mavumbini wewe utarudi."

    24 Baada ya kumfukuzia mbali Adamu, Mungu akaweka makerubi mashariki ya Bustani ya Edeni, pamoja na upanga wa moto ukimulika huku na huko kulinda njia ya kuuendea mti wa uzima.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.